5 Januari 2019 - 09:00
Marekani yapeleka wanajeshi   Congo

Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa nchi yake imewapeleka wanajeshi 80 mjini Libreville, Gabon, kuwalinda raia wa Marekani na ubalozi wa Marekani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa nchi yake imewapeleka wanajeshi 80 mjini Libreville, Gabon, kuwalinda raia wa Marekani na ubalozi wa Marekani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Katika barua aliyowasilisha Bungeni, Trump alisema wanajeshi Zaidi huenda wakapelekwa katika eneo hilo kutokana na uwezekano wa kuzuka maandamano yenye ghasia.

Barua ya Trump imesema wanajeshi hao "watabaki katika eneo hilo hadi hali ya usalama katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo utakapokuwa imara na uwepo wao usihitajike tena.”

Siku ya Alhamisi Wizara ya Mambo ya Nchi za Kigeni ya Marekani ilitoa wito kwa Tume ya Uchaguzi – CENI kuhakikisha kuwa kura zinahesabiwa kwa umakini na kutishia kuwawekea vikwazo watakaohujumu mchakato huo au kutishia Amani na utulivu wa nchi hiyo.

Ulaya na Afrika zaongeza mbinyo

Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika ziliiongezea mbinyo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, zikiitaka iheshimu matakwa ya wapiga kura wakati muda wa mwisho wa kutoa matokeo ukikaribia.

Kuna ongezeko la matarajio kuwa wasimamizi wa uchaguzi watachelewesha matokeo ya mwanzo yanayotarajiwa Jumapili – hatua inayoweza kuongeza hofu katika nchi hiyo isiyokuwa na utulivu.

"Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo iko katika wakati wa kihistoria kuelekea mpito wa kidemokrasia,” umesema Umoja wa Ulaya. Umetoa wito kwa maafisa kuhakikisha matokeo yananayosubiriwa yatatimiza matakwa ya wapiga kura. Ombi sawa na hilo limetolewa na Umoja wa Afrika – AU baada ya kupewa tathmini kutoka kwa mkuu wa timu ya uangalizi wa uchaguzi yenye wanachama 80.

Wapinzani wahofia wizi wa kura

Kama ilivyo kawaida kwa kwa Upinzani nchini humo unahofia kuwa matokeo hayo huenda yakafanyiwa uchakachuaji ili kumpa ushindi mtu ambaye Rais Joseph Kabila anapendelea awe mrithi wake, waziri wake wa zamani wa mambo ya ndani Emmanuel Ramazani Shadary. Anakabiliwa na wapinzani wawili wakubwa – Martin Fayulu, mkurugenzi wa zamani wa kampuni ya mafuta aliyejitosa saisani, na Felix Tsisekedi, mkuu wa UDPS, chama kikongwe kabisa na kikubwa cha upinzani nchini humo. Mpaka sasa wapinzani nchini Congo wanandaa vurufu kwa wananchi kwa kuwaaminisha kuwa kunawizi wa kura umetokea.

Mwisho wa habari / 291